May 26, 2017



Kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya michuano ya Azam Sports Federation Cup HD msimu wa 2016/17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Ahmed Kikumbo wa Dodoma kuwa mwamuzi wa mchezo wa fainali kati ya Simba SC na Mbao SC utakaofanyika Uwanja wa Jamburi Mei 27, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni.

Kikumbo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha. 

TFF inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna wao pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa kila upande.

Alfred Lucas Mapunda

Ofisa Habari na Mawasiliano TFF

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic