July 20, 2017


Baada ya kukwama jijini Dar es Salaam, hatimaye Msuva ameondoka kwenda Rwanda kuungana na kikosi cha Taifa Stars.

Stars iko jijini Kigali kuivaa Rwanda keshokutwa katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Chan. Katika mechi ya kwanza mjini Mwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Awali, Msuva alipanga kwenda Rwanda, jana alifika hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKIA), lakini baadaye alirejea nyumbani.

Lakini leo amefanikiwa kuondoka kwenda Rwanda kuongeza nguvu katika kikosi cha Stars.


“Kweli nimefanikiwa, nitaondoka leo jioni,” Msuva aliiambia SALEHJEMBE leo mchana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic