August 21, 2017



Na Saleh Ally
LIGI Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga imeanza kutimua vumbi kuanzia Ijumaa, jana Jumamosi, ikionyesha safari mpya imeanza.

Huu ni msimu wa 2017-18, wa ligi hiyo ikiwa imeanza na takwimu zinazoonyesha kuna nafasi ya Bayern Munich na Borussia Dortmund kutawala tena lakini inawezekana zikazaliwa timu nyingine mbili zitakazofanya vizuri.

Kawaida ya Bundesliga imekuwa ikitengeneza timu moja au mbili kila msimu baada ya msimu mmoja unaopita kama ulivyoona, RB Leipzig ilivyoshangaza msimu uliopita kwa kushika nafasi ya pili katikati ya Bayern Munich na Dortmund. Lakini msimu huu imeanza kwa kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa wakongwe wengine Schalke.

 Ligi hiyo ina timu 18 tu, na mbili huteremka na wameamua ibaki hivyo wakitaka kuona wachezaji wanakuwa na nafasi ya kushiriki michuano mingine na pia kupumzika.

Takwimu za Bundesliga ambayo kwa hapa nchini inaonyeshwa kupitia StarTimes zinaonyesha katika mechi hizo za siku mbili, tayari 71%, imekwenda kwa ushindi wa mechi za nyumbani ikionyesha walio nyumbani wamekuwa na uhakika zaidi.



 Lakini wako waliokuwa ugenini, hawakuwa na uhakika baada ya kuonyesha kuna 29% kushinda ugenini ikiongozwa na kigogo Dortmund walioshinda 3-0, dhidi ya Wolfsburg iliyokuwa uwanja wa nyumbani.

Yamefungwa mabao 14 katika mechi hizo za siku mbili ambayo yanatengeneza wastani wa 2.00, kwa mabao ya kufunga ambao kama utaendelea utaifanya Bundesliga kuendelea kuwa bora zaidi katika suala la takwimu.

Mashabiki wengi wa soka huenda wamekuwa hawajui kuhusiana na Bundesliga kwa kipindi kirefu na kusubiri kuziona timu za Ujerumani zinapoingia katika michuano ya Ulaya kama Europa League au Champions League.
Mara kadhaa, timu za Ujerumani ndiyo zimekuwa mwiba kwa timu za Hispania kama Real Madrid au Barcelona. Lakini mwisho zimepoteza mwelekeo wa kufanya vizuri zaidi.

Lakini bado Bundesliga inabaki kuwa ligi bora kwa uchezaji uwanjani kwa maana ya takwimu zinazoonyesha timu zao zinapocheza, muda mwingi zaidi mpira huchezwa badala ya kuwa nje wa uwanja.

Asilimia 94 ya mechi, mpira huwa uwanjani katika Bundesliga kuliko La Liga ambao ni 91%, England 88% na Ufaransa 87%.

 Bado ndiyo ligi inayoingiza watu wengi zaidi huku klabu ya Dortmund ikitamba zaidi kwa mashabiki wengi zaidi kushuhudia mechi za timu hiyo uwanjani.


Timu pekee imekuwa ikishindana na Dortmund ni Barcelona ambayo misimu miwili kabla iliongoza kabla ya Dortmund kurejea katika kiti chake msimu uliopita na inaonekana huenda ikaendelea na nafasi hiyo msimu huu kwa Barcelona kidogo inaonekana kudorora.
Pamoja na kuonekana Bundesliga nguvu inatumika sana, lakini ni mchanganyiko wa juu zaidi wa akili na nguvu. Hivyo kuifanya iwe ligi iliyokamilika kwa kuwa kama England ungesema nguvu, Hispania ukasema akili lakini Bundesliga inajumlisha vyote.
Kwa kuwa StarTimes wamekuwa wakiionyesha ligi hiyo, huenda mashabiki wanaweza kuangalia burudani ya soka la Ujerumani na kupima kwamba ubora ukoje.

Huenda vigumu kuangalia ligi bila kuvutiwa na timu gani. Lakini ukiacha mazoea, rahisi kuchagua timu katika Bundesliga baada ya kuiangalia uchezaji wake.

Burudani ya soka ni kubwa sana katika Bundesliga, kinachotakiwa ni kuondoa mazoea kwa kila mmoja kuamini akitaka kuangalia mpira ni lazima aangalie Premier League au La Liga kidogo.
Unaweza kujifuza zaidi katika Bundesliga kwa kuwa ni mpira wa nguvu na akili. Ni mpira unaochezwa muda mwingi uwanjani wachezaji wakiwa na ‘option’ kwa kuwa beki badala ya kubutua au kutoa nje, basi angeamini kucheza pasi akijiamini kwa kushirikiana na wenzake hadi kuutoa mpira katika hatari.
Bayern na Dortmund wameanza vizuri kwa maana ya kushinda mechi za kwanza za Bundesliga. Je, unafikiri hakuna anayeweza kuibuka na kuwa mfalme mbele yao? Basi endelea kufuatilia Bundesliga kwa ukaribu, ninaamini hautajilaumu na utajifunza mengi kuhusiana na soka huku uking’amua kuna utamu fulani ulikuwa ukiuokosa kwa kuwa hukuwahi kuthubutu kuangalia Bundesliga.


MATOKEO:
IJUMAA
Bayern 3-1 Leverkusen

JUMAMOSI
Hamburger SV 1 Vs  0 FC Ausgburg
Hertha 2 Vs 0 VfB Stuttgart
Hoffenheim 1 Vs 0 Werder
Wolfsburg 0 Vs 3 Dortmund
Mainz 0 VS 1 Hannover

Schalke 2 VS 0 RB Leipzig

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic