August 24, 2017


Muda mchache baada ya Simba kukabidhiwa Ngao ya Jamii iliyoibeba leo, gumzo limezuka hasa mitandaoni.

Simba imeshinda kwa mikwaju 5-4 ya penalti  dhidi ya Yanga na kubeba Ngao ya Jamii. Ngao hiyo, ikakabidhiwa na Rais mpya wa TFF, Wallace Karia kwa nahodha wa Simba, Method Mwanjale.

Lakini kitendo cha kukosewa neno Shield na kuwa Sheild, kimezua gumzo kubwa kwa wadau wa soka.

Wengi wamelaumu TFF kutokuwa makini au kufanya ukaguzi baada ya kuwa wamekabidhiwa ngao hiyo.

Blog ya SALEHJEMBE inaamini kwa wanadamu, kukosea ni jambo la kawaida. Lakini kwa kitu kama ngao, umakini zaidi unahitaji.

USHAURI:
Ushauri wa blog ya SALEHJEMBE, hata kama makosa ya kibinadamu yanaweza kutokea. Suala la kuandika kwa Kiswahili ni bora zaidi kuliko Kingereza.


Hivyo mara nyingine, ngao hiyo iandikwe hivi: “Ngao ya Jamii”.

1 COMMENTS:

  1. Naunga mkono ushauri wa kuandika kwa Kiswahili kwani ni moja ya njia za kukitangaza kiswahili duniani kote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic