August 21, 2017




Cosmas Kapinga ambaye kwa sasa ni meneja wa Simba, ametoa ufafanuzi kuhusiana na ile ishu ya taarifa za  Mohammed Zimbwe ‘Tshabalala’ kuzimia takribani dakika tatu uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Gulioni.

Kapinga ambaye kitaaluma ni daktari, amesema Zimbwe alianguka na kupata maumivu makali ya bega hivyo kumfanya aonekana kama ambavyo waandishi walianza kuamini alizimia.

"Alikuwa na maumivu makali sana ya bega, hakuzimia dakika tatu kama ilivyoelezwa. Lakini alilazimika kutulia kwa muda wakati akipata matibabu.

"Unajua kama mchezaji atazimia dakika tatu, basi atatakiwa kupumzika kwa siku sana. Lakini unamuona Tshabalala yuko na wenzake.

"Nafikiri waandishi walipaswa kuwa makini zaidi katika kuangalia hilo," alisema Kapinga.

Kwa maelezo hayo ya Kapinga, maana yake Zimbwe yuko fiti kabisa na itakuwa ni uamuzi wa mwalimu Joseph Omog acheze au la.

Taarifa za awali zilieleza hivyo, kuwa Zimbwe alizimia wakati wa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya Ngao ya Jamii ambayo Simba inakutana na Yanga, Jumatano saa 11 jioni.


Tukio hilo lilitokea zikiwa zimebaki siku mbili tu kabla ya timu hiyo kukutana na mahasimu wao Yanga, katika mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Ilikuwa ni katika mchezo dhidi ya Gulioni ambao Simba ilishinda 5-0, ukiwa ni ushindi wake mkubwa tangu waanze maandalizi ya msimu huu.

Zimbwe alipatwa na tatizo hilo katika dakika ya 86 baada ya kuchezewa rafu katika eneo la 18 alipokuwa akishambulia. 

Beki huyo alianguka ghafla kisha akatulia, hatua iliyowashtua wachezaji wenzake ambapo kiraka Erasto Nyoni, Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto walimkimbilia haraka kumpa huduma kabla ya daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe kuingia kuokoa jahazi akiongozana na Kapinga pamoja na mratibu Abbas Ally "Gazza" naye akaingia uwanjani pia ili kupata uhakika wa kilichokuwa kinaendelea.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic