August 21, 2017


Kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima alikuwa kivutio kwa mashabiki wa soka wakati Simba ikirejea nchini kutoka Zanzibar.

Kikosi kamili c ha Simba kimetua jijini Dar es Salaam leo tayari kwa mechi dhidi ya Yanga.

Yanga itaivaa Simba keshokutwa Jumatano katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na wachezaji wengi wa Simba kutoka ndani ya enero la uwanja wa ndege, mashabiki bado walionekana na hamu ya kumuona Niyonzima.


Baadaye Niyonzima alitoka na wengi wakamshangilia kwa nguvu, huku baadhi wale wa Simba wakiwazodoa wenzao wa Yanga kuwa wamepoteza kifaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic