August 19, 2017




Ndanda FC inatarajiwa kufanya tamasha lao kubwa la Ndanda Day litakalofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex uliokuwepo Chamazi, Mbagala jijini Dar Salaam, kesho. 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo iingie udhamini   wa mwaka mmoja na  Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye WhiteSands, Mbezi Beach Dar,  Mkurugenzi wa Masoko wa Ndanda, Peter Simon alisema, siku hiyo wamepanga kucheza mchezo wa kirafiki majira ya saa kumi kamili jioni dhidi ya Ruvu Shooting. 

Simon alisema, siku hiyo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wanamuziki wa bongo fleva ambao ni Jay Mo,  Juma Nature na Amini.

"Uongozi wa Ndanda tumepanga kutamburisha wachezaji wetu wapya ambao tumewasajili na benchi letu jipya la ufundi hiyo kesho. 

"Tumepanga tamasha letu la Ndanda Day iwe tofauti kwa maana la kuwa kubwa na kuvutia kwa mashabiki wetu wa Ndanda waishio Temeke na Mbagala na tumechagua kufanyia huko kwa sababu wengi wa Ndanda wapo maeneo hayo. 


"Hiyo kesho kabla ya shuguli asubuhi tutanya shughuli za kijamii kwa kwenda Hospitali ya Temeke wodi ya wazazi huku sherehe ikianza asubuhi saa nne, "alisema Simon.

6 COMMENTS:

  1. Kwa hili la NDANDA DAY uongozi wa timu ya Ndanda umefanya ubunifu mkubwa kuwa hii Ndanda Day itaongeza idadi ya wapenzi na mashabiki wa timu ya Ndanda

    ReplyDelete
  2. Kwa hili la NDANDA DAY uongozi wa timu ya Ndanda umefanya ubunifu mkubwa kuwa hii Ndanda Day itaongeza idadi ya wapenzi na mashabiki wa timu ya Ndanda

    ReplyDelete
  3. Hv Ndanda ni Timu ya Dar au Mtwara?Hv wangefanyia Mtwara si ingekuwa bora zaidi ya Chamazi. Hapa tumekosa ubunifu. Sidhan kàma Ndanda kwa Dar ni sahihi katika upatajwa wa washabiki

    ReplyDelete
  4. Ndanda day kifanyika Chamazi Dar, sio mtwara??? Halidumu hilo na ndio naamini kweli kuna ndanda dar na ndanda mtwara

    ReplyDelete
  5. Hakika wamekosea ilipaswa kufanyika mtwara na si dar nahisi maamuzi Yao yamefanyika kishabiki na si kufata maudhui halisi ya ndanda day

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic