September 20, 2017


Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Emmanuel Martin amerejea kazini akiwa fiti kabisa.

Martin alishindwa kumaliza mechi kati ya Yanga dhidi ya Majimaji ya Songea baada ya kugongwa kwa nguvu na beki wa Majimaji.

Mkanda wa video unaonyesha beki huyo akimgonga Martin kwa makusudi hali iliyosababisha apoteze fahamu.

Lakini leo amefanya mazoezi na wenzake katika Uwanja wa Uhuru akionekana yuko fiti kabisa.


Maana yake, Kocha George Lwandamina ana nafasi ya kumtumia kama atamhitaji katika mechi ifuatayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic