September 19, 2017




Kiungo wa Simba, Haruna Hakizimana Niyonzima, sasa yuko fiti na anachosubiri ni uamuzi wa Kocha Joseph Omog kama acheze mechi dhidi ya Mbao FC au la.

Niyonzima ambaye alikuwa majeruhi, alikuwa amefanya mazoezi siku mbili kabla ya Simba kuivaa Mwadui FC na kushinda kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Leo, Niyonzima amejifua na wenzake kwenye Uwanja wa Alliance katika kitongoji cha Mahina jijini Dar es Salaam.

Simba iko jijini humo kwa ajili ya mechi yake ya kesho dhidi ya Mbao FC itakayopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.



1 COMMENTS:

  1. Alliance katika kitongoji cha Mahina Jijini Dar es Salaam???????

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic