September 26, 2017

Ukisema kuwa kampuni ya Startimes inaithamini lugha ya Kiswahili utakuwa haujakosea.

Maana imetangaza msimu wa pili wa Shindano la Vipaji vya Sauti linaloendeshwa na Kampuni ya StarTimes Tanzania, umezinduliwa rasmi leo Jumanne.

Msimu huo wa pili umekuja baada ya msimu wa kwanza kuonyesha mafanikio makubwa ambapo washindi saba kati ya kumi walienda Beijing nchini China kufanya kazi ya kuingiza sauti za Kiswahili kwenye tamthiliya za Kichina.

Usaili wa mwaka huu utafanyika Zanzibar, Mwanza na Dar es Salaam, ambapo Zanzibar itakuwa Septemba 30, Mwanza ni Oktoba 7 na Dar es Salaam Oktoba 14, huku fainali ya kuwapata washindi wa jumla ikitarajiwa kuwa Oktoba 28, mwaka huu.

Meneja wa Masoko na Mahusiano wa StarTimes, Juma Suluhu, amesema: “Msimu wa kwanza ulikuwa na mafanikio makubwa kwani washindi walienda China kufanya kazi za kuingiza sauti za Kiswahili kwenye tamthiliya za Kichina ambazo zinaonyeshwa sehemu mbalimbali ikiwemo katika chaneli yetu ya Star Swahili.

“Lengo la shindano hili ni kukuza Lugha ya Kiswahili ambayo tangu kuanza kwake tumeona matunda kwa sababu Wachina wengi wameanza kujifunza Kiswahili.”

MSIMU wa pili wa Shindano la Vipaji vya Sauti linaloendeshwa na Kampuni ya StarTimes Tanzania, umezinduliwa rasmi leo Jumanne.

Msimu huo wa pili umekuja baada ya msimu wa kwanza kuonyesha mafanikio makubwa ambapo washindi saba kati ya kumi walienda Beijing nchini China kufanya kazi ya kuingiza sauti za Kiswahili kwenye tamthiliya za Kichina.

Usaili wa mwaka huu utafanyika Zanzibar, Mwanza na Dar es Salaam, ambapo Zanzibar itakuwa Septemba 30, Mwanza ni Oktoba 7 na Dar es Salaam Oktoba 14, huku fainali ya kuwapata washindi wa jumla ikitarajiwa kuwa Oktoba 28, mwaka huu.

Meneja wa Masoko na Mahusiano wa StarTimes, Juma Suluhu, amesema: “Msimu wa kwanza ulikuwa na mafanikio makubwa kwani washindi walienda China kufanya kazi za kuingiza sauti za Kiswahili kwenye tamthiliya za Kichina ambazo zinaonyeshwa sehemu mbalimbali ikiwemo katika chaneli yetu ya Star Swahili.

“Lengo la shindano hili ni kukuza Lugha ya Kiswahili ambayo tangu kuanza kwake tumeona matunda kwa sababu Wachina wengi wameanza kujifunza Kiswahili.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic