October 23, 2017





Michuano ya mpira wa kikapu ya StarTimes Supercup, ilihitimishwa jana Jumapili kwa kupigwa mchezo wa fainali ambapo JKT iliibuka na ushindi wa vikapu 78-58 dhidi ya Oilers. Mechi hiyo ilipigwa katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar, huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe.


Kampuni ya StarTimes ambayo ndiyo iliyodhamini michuano hiyo, ilitoa zawadi kwa washindi ambapo bingwa JKT walikabidhiwa kitita cha Sh milioni mbili, medali za dhahabu na kikombe, huku washindi wa pili, Oilers wakikabidhiwa medali za fedha, kikombe na kitita cha Sh milioni moja. 

Kwa upande wa washindi wa tatu ambao ni Tanzania Prisons, waliambulia medali za shaba pekee.


Kabla ya kupigwa mchezo wa fainali, ilichezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ambapo Tanzania Prisons iliibuka na ushindi wa vikapu 67-66 dhidi ya Savio.


Katika michuano hiyo, Baraka Sadick wa JKT, aliibuka Mchezaji Bora wa Michuano (MVP), Mfungaji Bora ni Emmanuel Mwendo wa Prisons na Mlinzi Bora ni Juma Kissoky wa Oilers, wote hao walikabidhiwa medali za dhahabu na simu za kisasa ‘smartphones’ kutoka StarTimes.


Ikumbukwe kuwa, michuano hiyo imefanyika tena mwaka huu baada ya kupita takribani miaka kumi ambapo mara ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka 2006 na JKT kuibuka bingwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic