October 20, 2017



Kocha wa zamani wa Mwadui FC, Ali Bushiri amelalamika klabu ya Mwadui FC kuendelea kukaa kimya na mshahara wake wa mmoja.



Bushiri maarufu kama Shilton amesema Mwadui FC hawakumlipa fedha hizo akiamini wangefanya hivyo baadaye.

“Hadi sasa hawajanilipa mshahara wa mwezi mmoja na nimekuwa nawasiliana na uongozi, wanasema wanatanilipa.

“Nimeendelea na subira lakini naona wanaendelea kuwa kimya bila ya kusema lolote. Unajua nilifutwa kazi nikiwa Zanzibar nisingeweza kurudi huko na mshahara wangu sikuwa nimelipwa.”

Hivi karibuni, Bushriki alisema iwapo timu hiyo itamhitaji basi imtimue kocha mwingine aliyeoko sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic