October 17, 2017




Beki wa Simba, Salim Mbonde atakosa takribani mechi tatu hadi nne.

Mbonde aliumia katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo Simba ililazimisha sare ya bao 1-1 katika hatua za mwisho.

Simba itashuka dimbani kuivaa Yanga Oktoba 28 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Beki huyo aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar, aliumua katika mechi hiyo hali iliyomlazimu kocha Joseph Omog amtoe na kumuingiza Juuko Murshid.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema: "Kwa hali hiyo maana yake hawezi kucheza mechi dhidi ya Yanga."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic