October 18, 2017



Uongozi wa Yanga tayari umeanza harakati za kutakakukiongezea nguvu kikosi chake katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kutokana na kuvutiwa na uwezo wa viungo wawili wa Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa pamoja na Mohammed Issa ‘Banka’ uongozi huo tayari umeanza mikakati ya kuhakikisha unawasajili wachezaji hao katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa mwezi Novemba.

Baadhi ya viongozi wa Yanga walionekana wakiwa katika majadiliano makali kuhusiana na wachezaji hao na mwisho wa siku wakakubaliana kuanza mazungumzo rasmi.

“Nimewafuatilia wachezaji hao mechi mbili hivi hakika ni wazuri na wanatufaa kabisa kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu yetu ya kiungo,” alisema mmoja kati ya viongozi hao huku mwingine naye akisema kuwa.

“Jambo la msingi hapa ni kuanza mazungumzo mapema lakini pia tuwatafute watu wao wa karibu ili tuzungumze nao waweze kutusaidia na ikiwezekana katika dirisha dogo la usajili tuwasajili.”


Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila kama yupo tayari kuwaachia ambapo alisema kuwa: “ Mtibwa Sugar sisi hatujawahi kuzuia mchezaji kama watakuja na kuzungumza na viongozi na wakifikia makubaliano basi watawachukua lakini kwa sasa wana mkataba wa muda mrefu na klabu yetu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic