November 17, 2017



Kiungo mkabaji wa Yanga, Papy Tshishimbi sasa atalazimika kutumia viatu maalum, vyenye meno madogo.

Uamuzi wa kutumia viatu hivyo, si wake. Bali ni kutoka kwa Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu akimtaka kutumia viatu maalumu.

Kiungo huyo raia wa DR Congo, alipata majeraha hayo katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi Jumatano asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mkongo huyo ambaye alijiunga na Yanga kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara alipata majeraha hayo akiwa ametoka kuugua malaria iliyomuweka nje ya uwanja kwa siku tatu.

Bavu alisema kiungo huyo mara baada ya kupata majeraha hayo juzi alipatiwa matibabu ya haraka ili kuhakikisha anarejea uwanjani kwa haraka kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Mbeya City.

Bavu alisema, kiungo huyo anaendelea vizuri na matibabu yake na leo anatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake katika kujiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City.

Aliongeza kuwa, amemtaka kiungo huyo kutumia  viatu visivyokuwa na meno ‘njumu’ kuhofia kupata majeraha mengine kutokana na mazingira ya uwanja wanaoutumia kuwa mgumu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic