November 24, 2017



 Emmanuel Okwi sasa atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wa Simba kuhakikisha anarejea katika hali yake haraka.

Daktari wa Simba atafanya hivyo kuhakikisha Okwi anapona enka na kurejea katika hali yake ili kurudi uwanjani.


Okwi ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi kuu kwa sasa kutokana na kuwa na mabao nane akifuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons ambao wote wana mabao sita.

Okwi alipata majeraha ya enka kabla ya mechi dhidi ya Prisons ya Mbeya ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa timu hiyo umemkabidhi jukumu Dk Yasin Gembe kuhakikisha anakuwa na uangalizi wa hali ya juu kwa mchezaji huyo kutokana na majeraha aliyonayo.

“Uongozi umetaka Okwi awe chini ya uangalizi wa  dokta kutokana na majeraha aliyonayo, kwa kuwa ndiye kinara wa mabao, hivyo ni vyema akaangaliwa ili aweze kupona kwa haraka na kurejea mzigoni,” alisema mtoa taarifa huyo.

Simba inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 22 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 20  ambapo timu zote zimeshuka dimbani mara 10, hali ambayo inaonyesha ni jinsi gani ligi imekuwa ngumu. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic