December 14, 2017




Suala la Serikali kuweka wazi kwamba mfumo wa umiliki wa hisa katika uwekezaji katika klabu ya Simba, limeanza kuzua mijadala kila upande ukijaribu kutetea unachoona sahihi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema uwekezaji unapaswa kuwa asilimia 49 kwa muwekezaji Mohammed Dewji na 51 inabaki kwa wanachama.

Mwakyembe aliyasema hayo wakati alipojitokeza katika udhamini wa kampuni ya Biko kwa timu ya Stand United.

Kauli yake ilikuwa ni kufafanua baada ya wanachama wa Simba kupitisha uwekezaji wa asilimia 50 kwa 50.

Baada ya hapo, kumekuwa na mjadala mkubwa hasa mitandaoni, wengine wakiona sawa na wengine wakiona si sawa.

Mfumo wa 49 kwa 51 zaidi unatumika katika Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Awali, Dewji aliwahi kusema alikuwa akiweka Sh bilioni 20 ili kuwekeza kwa asilimia 51.

Baadaye ilionekana haiwezekani na mwisho makubaliano yakawa ni asilimia 50 kwa 50 lakini kauli hiyo ya serikali imeamsha mjadala mpya.

Wanaounga mkono wanaona ni sahihi wengi kuwa na nguvu jambo ambalo serikali inaamini lakini wengine wanaona anayetoa fedha pia ana haki ya kuwa na nguvu zaidi.




1 COMMENTS:

  1. MPIGA DILI TU, KAMA BIASHARA YA SOKA INALIPA SI AANZISHE TIMU? ANGEPEWA HATA 2%

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic