December 13, 2017



Taarifa zinaeleza kwamba, hivi sasa straika Mtanzania, Thomas Ulimwengu anasubiri barua kutoka katika timu yake ya AFC Eskilstuna ili ajiunge na timu nyingine katika usajili ujao wa dirisha dogo barani Ulaya unaoatarajiwa kufunguliwa Januari, mwakani.

Hivi karibuni, Ulimwengu alivunja mkataba na timu yake hiyo iliyokuwa ikicheza ligi kuu nchini humo kabla ya kushuka daraja msimu ulipomalizika hivi karibuni.
Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo, alisema baada ya taratibu zote za kuvunja mkataba kukamilika, wanachosuburi kwa sasa ni barua ya kuruhusiwa kuondoka klabuni hapo ili iwe rahisi kujiunga na timu yoyote.
“Nadhani haitakuwa ngumu wao kutupatia barua hiyo kwani makubaliano yaliyofanyika wakati wa kuvunja mkataba yalikuwa mazuri tu na wala hakukukuwa na shida yoyote ile.
“Matarajio yetu ni kuipata hivi karibuni kwani tunataka tuwahi usajili wa dirisha dogo ili kijana aweze kupata timu hukohuko Ulaya na sio kurudi Afrika. Kila kitu kikiwa vizuri, nitawajulisha ni timu gani atajiunga nayo,” alisema Kisongo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic