December 13, 2017




Wapinzani wa Simba na Yanga katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), wanatarajia kujulikana leo Jumatano ambapo ratiba itapangwa nchini Cairo, Misri.


Michuano ya Caf inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Februari mwakani huku Yanga ikitarajia kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita huku wapinzani wao Simba wakishiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho kutokana na kuibuka mabingwa katika michuano ya Kombe la FA, msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa tayari klabu hizo kongwe zimeshawasilisha usajili wa wachezaji wao Caf kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo.


“Tayari klabu zote za Simba na Yanga zimeshawasilisha majina ya usajili wa wachezaji wao wote Caf kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya klabu bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.


“Ratiba ya makundi inatarajiwa kupangwa leo’ nchini Misri hivyo tutapata fursa ya kutambua Simba itacheza na nani na Yanga itacheza na nani kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michuano hiyo.

“Kawaida usajili wa kimataifa katika michuano Caf lazima wataacha nafasi kwa ajili ya kuongeza wachezaji wengine hapo baadaye, kwa upande wa Simba na Yanga wamepeleka majina ya wachezaji wao wote waliowasajili lakini hawakufikia idadi ya wachezaji 30 ambayo ndiyo ya mwisho,” alisema Lucas.

Simba na Yanga zimekuwa zikifanya vizuri kila zinapokutana na timu nyingine, lakini zinapokutana na timu kutoka kwenye nchi za Kiarabu mambo huwa magumu, hivyo hawataki kabisa kukutana na hali hiyo.

Toimu vigogo ambazo Yanga hawataki kukutana nazo na zipo kwenye Klabu Bingwa Afrika ni Al Ahily, Esperance, Etoile du Sahel, TP Mazembe, Waydad Casablanca na ES Setif.

Simba wenyewe watakuwa wanakwepa kukutana na Zamalek, Enyimba, Raja Casablanca, Supersport United na USM Algier.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic