January 19, 2018



Yanga imeendelea kujifua leo huku kiungo wake, Thabani Kamusoko akiendelea na mazoezi binafsi.

Mazoezi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara yamefanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kamusoko alikuwa akiendelea na mazoezi binafsi ya kujifua pembeni ikiwa ni dalili njema kwamba atarejea hivi karibuni.

Kiungo huyo raia wa Zimbabwe amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu sasa huku Yanga ikiendelea kupambana.


Hata hivyo, Kamusoko amekuwa akionyesha uungwana kwa kuhudhuria mazoezi ya Yanga licha ya kwamba ni majeruhi. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic