January 19, 2018


Baada ya kuwa kero kutokana na kuchelewa kurejea nchini, Emmanuel Okwi amejiunga na Simba na mechi ya kwanza ambayo ilionekana ngumu dhidi ya Singida United, amepiga bao mbili.

Bao hizo mbili, Okwi amezirejesha kwao Uganda kwa kumzawadia mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni.

Pamoja na kuwa majeruhi lakini Okwi alilazimika kubaki Uganda baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili.

Zawadi hiyo kwa mwanaye imetolewa mara tu baada ya mechi ya jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Okwi akiwa shujaa wa mchezo huo katika ufungaji mabao.


Simba ilionyesha soka safi na kufanikiwa kuituliza Singida ambayo awali ilionekana ni hatari kubwa kwa Simba.

1 COMMENTS:

  1. Okwi ni mchezaji wa level ya juu hapa ncini yupo sharp kitu amabacho washambulisji wengi wazawa wanakosa. Inashangaza kuona Okwi ameridhika kufanya kazi Tanzania peke yake na kuacha offer nyingi za nje. Ikiwa Okwi aliwasumbua wa Egypt na kuwapachika bao hadi kuwa gumzo Cairo ni dhahiri kuwa Okwi ni miongoni mwa washambulisji mahiri katika ukanda wetu huu wa Africa lakini la kushangaza zaidi Simba ina mchango mkubwa katika makuzi ya soka ya Emanuel Okwi kitu ambacho wadau wengi wamekuwa hawakiongelei wanakuwa wanaizungumza simba na Okwi wakati wa matatizo tu. Wakati mwengine au wakati mwingi zaidi tatizo sio timu, tatizo ni vijana wetu. Utasikia aagh Simba na Yanga zinaharibu wachezaji kitu ambacho siku zote napingana nacho kwani wachezaji wanajiharibu wao wenyewe. Simba na Yanga zaidi zinawasaidia wachezaji katika mambo mengi tu. Mfano kimataifa na kibiashara mtu mwenye wafuasi wengi wa watu ikiwa kwenye mtanadao wa kijamii au siasa basi akikutangaza kwa watu wake basi kama kichwa chako kizuri basi upo uwezekano mkubwa wa mufanikiwa katika mambo yako. Sasa unapoizungumzia Simba na Yanga Tanzania au east Africa unazungumzia mamilioni ya watu. Miongoni mwa wafuasi wa vilabu hivi viwili kuna watu wana connection nyingi za kimaisha na kimaendeleo kama hawa vijana wetu wanaobahatika kufanya kazi katika timu hizi mbili wanajitambua wapo wapi basi tusingesikia lawama za Simba na Yanga zinaharibu wachezaji. Okwi ameichezea simba kwa muda tu kuliko wachezaji wengi na kiwango chake siku zote ni cha juu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic