February 21, 2018



(YANGA INASONGA MBELE KWA JUMLA YA MABAO 2-1)
FULL TIME
GOOOOOOOO Dk 90+2 St Louis wanapata bao hapa baada ya uzembe wa Yanga langoni mwao



DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90 Yanga inapata kona dakika za mwisho kabisa
Dk 89 shambulizi kali wanafanya St Louis, lakini Rostand anaonyesha yuko vizuri anadaka na kulala
Dk 89 Yanga wanaendelea kuonekana hawana haraka kwa kuwa uhakika sasa ni asilimia 99
Dk 87, Yanga wanaonekana wamerudi nyuma ili kumaliza game kwa ushindi wa 1-0
Dk 84 Rostand taratibu anaonyesha mbwembwe huku akidaka na kulala chini
Dk 83 Yanga inapata kona, inachongwa kibishooo na Ajibu na kipa anadaka kwa ulaini
Dk 82 sasa, Yanga wanaendelea kushambulia kama vile wanahitaji bao la pili haraka sana ambalo ni jambo zuri kwa timu hii ya Tanzania
Dk  79, alikuwa ni Rostand upande wa Yanga, tayari ameinuka baada ya kupata huduma ya kwanza
Dk 78 wachezaji wa St Louis na Yanga wanagongana hapa wakati wakiwania mpira. Wote wako chini pale na wauguzi tayari wameingia uwanjani
SUB Dk 77 Yanga inamwingiza Mwinyi Haji kuchukua nafasi ya Gadiel
Dk 75 Ajibu anawachambua mabeki watatu, lakini anakuwa na haraka katika umaliziaji, goal kick
Dk 74 Rostand anaruka juu kudaka, anautema. Hatariii lakini St Louis wanakosa, goal kick


Dk 73, Rostande analazimika kutoka nje ya eneo lake na kuokoa 
SUB Dk 72 Yannick Julie anaingia kuongeza nguvu upande wa St Louis
Dk 70 Bado milango ni migumu ingawa St Louis wanapata nafasi ya mashambulizi na Yanga wanapaswa kwua makini
Dk 68 Yanga wako pungufu mtu mmoja kwa kuwa Ngoyani yuko nje akipatiwa matibabu
Dk 66 Mkwaju mkali langoni mwa Yanga, unaokolewa na Yondani na kuwa wa kurusha
Dk 65, Daud anaachia mkwaju mkali kabisa inakuwa ni goal kick
Dk 63 St Louis wanaingia vizuri kabisa lakini Rostand yuko makini
SUB Dk 59 Makapu aliumia, ameshindwa kuendelea na nafasi yake inachukuliwa na Raphael Daud Loti
SUB Dk 57 St Louis wanafanya mabadiliko wanamuingiza Mellanie


KADI Dk 55, Makapu analambwa kadi ya njano baada ya kumgonga mshambuliaji wa St Louis
Dk 54, nusura Tshishimbi aipatie Yanga bao la pili lakini anadhibitiwa
Dk 54, Kessy tena mara nyingine kutokea katikati, anaachia mkwaju mkali, lakini hakulenga lango Dk 52 Makapu anafanya kazi ya ziada na kuukoa mpira, kona kwenye lango la Yanga, inachongwa goal
Dk 49, Kessy anaingia vizuri, safari hii anajaribu mwenyewe, goal kick
Dk 47, mpira mreefu kwenye lango la Yanga, Rostand anaruka na kudaka vizuri kabisa
45 St Louis wanaanza kwa kasi kubwa wakionekana wamepania kupata bao




HALF TIME
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
GOOOOOOOO Dk 45 sekunde kadhaa baada ya Ajibu kurejea uwanjani anaunganisha krosi safi kabisa ya Kessy na kuitanguliza Yanga ya Tanzania kwa bao moja
Dk 44 Ajibu amerejea uwanjani kuendelea na mchezo
Dk 43, St Louis wanaonekana wamehamia langoni mwa Yanga wakishambulia mfululizo
Dk 42, Ajibu alikuwa ameumia, ametolewa nje kwa ajili ya matibabu
Dk 38 Kessy anaingia vizuri hapa, anavutwa lakini mwamuzi msaidizi inaonekana hakuona, Kessy anahoji


Dk 36 Yanga wanapata nafasi nzuri kabisa lakini Buswita anaonekana kama mtu aliyechoka au mgonjwa hivi!!
Dk 34 St Louis nao wanafanya shambulizi la haraka, inakuwa ni kona, inachongwa hapa, Yondani anajitwisha na kuokoa
Dk 33 kona fupi inachongwa na Ajibu, Kessy anapiga mpira mkuubwa. Inaonekana hawa hawako makini
Dk 32, Martin anaachia mkwaju wa juujuu, unaokolewa na kuwa kona
Dk 30 Kessy anapiga pasi safi kwa gadiel, naye anapiga mkwaju unaokolewa na kuwa kona nyingine kwa Yanga, inachongwa kona fupi, inaokolewa
KADI Dk 29 Cannavaro analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 28, krosi nzuri ya Gadiel, St Louis wanaokoa lakini mpira anauwahi Ajibu anaachia mkwaju hapa, goal kick



Dk 27, mpira wa faulo, ni hatari lakini Rostand anaruka juu kabisa na kuudaka
Dk 26 Kessy anamuangusha kiungo wa St Louis, si mbalis ana karibu na lango lao
Dk 24 Martin anaachia mkwaju mkali unawababatiza walinzi wa St Louis unatoka na kuwa wa kurushwa
Dk 19, St Louis wanapata kona ya kwanza baada ya kufanya shambulizi kali. Inachongwa hapa lakini Tshishimbi anaokoa hapa
Dk 17, Yanga inapata kona nyingine baada ya krosi safi ya Ajibu. Ajibu huyohuyo anachonga kona safi kabisa lakini offside
Dk 13, kona inachongwa lakini haina manufaa hata kidogo
Dk 13, Yanga wanafanya shambulizi kali na kupata kona ya pili


Dk 12 sasa, Yanga wanaonekana kucheza vizuri katika eneo la katikati lakini hawajawa vizuri katika umaliziaji
Dk 9, St Louis wanafanya shambulizi jingine kali, shuti linapigwa, mpira unambabatiza Kessy na unaokolewa
Dk 7, shambulizi jingine la Yanga, Ajibu anatishwa lakini ni goal kick
Dk 6 Yanga wanapata kona ya kwanza, inachongwa vizuri lakini St Louis wanaokoa
Dk 4 mpira mrefu wa Tshishimbi lakini Martin anashindwa kuuwahi
Dk 2, Yanga wanafanya shambulizi la kwanza lakini Yanga bado wako makini

Dk 1, St Louis imeanza kwa kasi ikionekana wamepania kupata bao la mapema

1 COMMENTS:

  1. Hongera Yanga. Muhimu mmeshinda mnaingia hatua ya pili. Nimeuangalia mchezo. Haukuwa wa ushindani sana pengine ni nzuri kwakuwa wachezaji wana michezo muhimu ya Ligi na Azam FA mbele yao hivyo hawakujituma saana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic