February 19, 2018




Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji bado haijaimarika vizuri baada ya kulazimika kufanyiwa upasuaji mwingine mdogo na kuwekewa chuma katika mshipa mmoja wa damu.

Habari za uhakika zinaeleza, katika ya mwezi uliopita, Manji alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kabla ya kufanyiwa upasuaji huo mdogo.

Kutokana na upasuaji huo, Manji amewekewa vyuma viwili ndani ya mwaka mmoja kwa kuwa Februari mwakani akiwa katika misukosuko baada ya kutangazwa alikuwa anatuhumiwa na uuzwaji wa madawa ya kulevya, alifanyia upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Chanzo kimeeleza, kwamba madaktari wameeleza si salama kwa Manji kufanyiwa upasuaji wa namna hiyo ndani ya mwaka mmoja.

“Angalau miaka minne au mitatu, lakini yeye ni mwaka mmoja amewekewa vyuma mara mbili. Daktari ameonya kwamba si jambo jema kiafya,” kilieleza chanzo.

“Hata hivyo, wamekuwa wakifanya siri sana. Unajua amekuwa na presha sana kutokana na matatizo yanayomuandama. Kuna wafanyakazi zaidi ya 4,750 waliokuwa wanafanya kwa Manji ilibidi waondolewe maana kampuni zake zote zimefungwa.

“Hii inaonekana kumchanganya sana, ndiyo maana amekuwa akiumwa na alikatazwa hata kuzungumza na simu hadi wiki moja iliyopita.”

Juhudi za kumpata Manji zilifanyika na juzi jioni alipatikana, naye alipoulizwa akagoma kufafanua zaidi ya kuthibitisha kweli alilazwa.

“Ndiyo ninaumwa, nililazwa Aga Khan. Sasa mimi sipendi kuzungumza mambo yangu ya ugonjwa kwenye vyombo vya habari,” alisema.

Baada ya hapo, zilifanyika juhudi za kufika Aga Khan na kutaka kujua kutokana upasuaji aliofanyiwa, inakuwaje kuhusiana naye.

Aga Khan walionekana kuwa wagumu  na walisisitiza mzungumzaji huwa hafanyi kazi Jumapili na hata juhudi za kupata namba yake zilipofanikiwa, ilionekana bado ni vigumu kumpata.

Baada ya mwandishi wa Championi kufika Aga Khan, mmoja wa wafanyakazi alimpa ushirikiano huku akionyesha ni mwenye hofu na alitaka kujua kipi hasa gazeti lilitaka kukijua.

Alipoelezwa alisisitiza kuwa msemaji anapumzika siku hiyo na kumtaka mwandishi kuondoka na kurejea kesho yake.


SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic