February 19, 2018





Uongozi wa Simba umesema kipa wake Aishi Manula anaendelea vizuri na kuna asilimia 90 za yeye kucheza mechi ya kesho dhidi ya Gendamarie.

Simba iko nchini Djibouti tayari kuivaa Gendamarie katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho. Simba ilishinda kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza jijini Dar.

Benchi la ufundi limeeleza kwamba kinachomsumbua Manula baada ya kuupia leo ni kidole.

"Daktari amesema hadi asubuhi atakuwa na la kusema ingawa anaona kwa asilimia tisini ana nafasi ya kucheza. Kama hakitakuwa kimevimba asubuhi, basi atakuwa tayari kucheza kama akipangwa na mwalimu.

"Tayari alianza kupatiwa huduma pale uwanjani na baadaye usiku huu na tunaamini ataamka vizuri," kilieleza chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic