February 17, 2018




Simba haijafanya mzaha licha ya kuonekana Gendamarie ni timu dhaifu baada ya kuitungua mabao 4-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu hizo zinarudiana Jumanne na Simba tayari imetuma mwakilishi kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri.

Imeelezwa mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo tayari ametua nchini humo ili kuweka mambo sawa.

“Amekwenda huko ili kujua mazingira na kila kitu. Unajua huko Djibouti si sehemu iliyozoeleka, vizuri kuwa na mtu mzoefu ambaye atajua nini kipo huko,” kilieleza chanzo.


Simba imeonekana haitaki kufanya mzaha licha ya kuanza kwa ushindi wa mabao 4-0 mjini Dar es Salaam.a

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic