February 25, 2018


Na George Mganga


Yanga imekuwa imesonga mbele katika mashindano ya Kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Majimaji FC, mechi ikichezwa katika Uwanja wa Majimaji.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi kwa pande zote mbili huku Majimaji wakiongoza kumiliki mpira, ulianza kutikiswa kwa nyavu za Majimaji kupitia Pius Buswita katika dakika ya 40.

Goli hilo la Buswita lilimaliza kipindi cha kwanza huku Yanga ikiwa mbele kwa matokeo ya 1-0.

Kipindi cha pili kilipoanza, dakika ya 52, Emmanuel Martin alifunga goli la pili kwa njia ya kichwa, akiunganisha krosi nzuri ya Hassan Kessy, na kufanya matokeo yawe mabao mawili kwa Yanga na sufuri kwa Majimaji.

Na katika dakika ya 61. Jaffar Mohammed, alifanikiwa kuipatia Majimaji FC bao la kusawazisha kwa njia ya kichwa na kufanya ubao wa matokeo kubadilika na kuwa 2-1.

Mpaka dakika 90 zinamaliza, Majimaji 1 na Yanga 2.

Kwa matokeo haya sasa Yanga imeingia hatua ya 8 bora ya Kombe la Shirikisho, na kuiondoa Majimaji FC ya mkoani Ruvuma.

1 COMMENTS:

  1. Majimaji wamejitahidi kwa mazingira waliyokuwa nayo kucheza bila wachezaji wao saba wa kutumainiwa ambao walisimamishwa kutokana na ukosefu wa nidhamu. Yanga ni timu bora hivyo ushindi huo wamestahili hongera Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic