September 20, 2018


















Kampuni maarufu zaidi ya ya Kubashiri Michezo Tanzania ya SportPesa, leo Alhamisi imezindua rasmi promosheni ya kuinua maisha kiuchumi ijulikanayo kwa jina la Shinda Zaidi na SportPesa itakayodumu kwa siku 100 ambapo mshindi atajishindia Bajaj RE mpya.

Promosheni hiyo ambayo imeanza kwa watakaobashiri mechi za leo Alhamisi kupitia SportPesa, kesho Ijumaa mshindi wa kwanza anatarajiwa kukabidhiwa zawadi yake hiyo ya bajaj.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas, alisema: “Mwaka jana tuliendesha promosheni kama hii ambayo ilikuwa ikiitwa Shinda na SportPesa ambapo tulitoa bajaj 100 kwa washindi wetu.

“Washindi walitoka katika mikoa 23 ya Tanzania na waliweza kubadilisha maisha yao kwa kujiongezea kipato cha kila siku kupitia bajaj ambazo wengi walizitumia kwa biashara. Nia yetu SportPesa ni kuendelea kuinua na kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo.

“Sasa kupitia Shinda Zaidi na SportPesa, tutaweza kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kupitia bajaj na zawadi zingine kwa muda wa siku 100. Ninayo furaha kuwa Sportpesa imekuwa ikibadilisha maisha ya Watanzania kiuchumi kwa kupitia michezo.

“Tangu Mei 2017 ambapo Kampuni ya SportPesa ilianza kufanya shughuli zake hapa nchini, kampuni hii imeweza kutoa Sh bilioni 26.5 kama zawadi kwa Watanzania wanaobashiri kupitia SportPesa.”

Katika hatua nyingine, Tarimba alisema Kampuni ya SportPesa imekuwa msaada mkubwa kwa jamii hapa nchini kutokana na mambo inayoyafanya ikiwemo mwaka jana kuileta timu ya Everton, kudhamini timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara na kuukarabati Uwanja wa Taifa ambao ulitumia Sh bilioni 1.4.

Naye Meneja Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya, alisema ili ushiriki kwenye promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa na kushinda Bajaj RE mpya, mteja anatakiwa kubashiri kwa kuanzia Sh 1000 tu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Submean Auto Ltd ambao ndio wasambazaji wa Bajaj RE, Venkatesh K-Business, alisema: “Sisi Submean Limited tunatoa waranti ya miezi 12 kwa Bajaj RE 4S ili kuonyesha imani yetu kwa bidhaa zetu. Natoa rai yangu kwa Watanzania kubashiri kupitia SportPesa na kuwa washindi.”

Kampuni ya SportPesa, ndiyo kampuni ya kubashiri michezo inayoongoza Afrika ambapo inatoa bashiri zaidi ya 500 kila siku kwa wateja wake na wapenzi wa soka kujishindia zawadi kemkem.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic