September 20, 2018






Uongozi wa Simba umekutana na wachezaji wake na kuwaeleza kile wanachoamini kinatakiwa ambacho ni ushindi dhidi ya Mbao FC, leo.


Wachezaji wa Simba nao wameahidi kufanya vema wakijua kuwa mechi dhidi ya Mbao FC hasa ikiwa nyumbani mara nyingi ni ngumu kwao.


Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wachezaji wameelewa kinachotakiwa nao wamewaahidi furaha.


“Tumewaambia wachezaji kinachohitajika leo na wameahidi furaha kwa Wanasimba, endeleeni kutuunga mkono na kutuombea,” alisema Manara alipozungumza na SALEHJEMBE BLOG.


“Always Simba ni moja na tutabaki hvyo. Tukishinda ni Simba na vyovyote vile ni Simba, 
Inshaalla tutashinda,” aliongeza Manara.


Simba wanawavaa Mbao FC ambao tayari wana pointi saba sawa na wao baada ya kucheza mechi nne za Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic