Wapi
anakoelekea Arsene Wenger kutoka alipo sasa? Inaonekana kama mashabiki wa Arsenal nchini England wanaweza kuacha kuingia kwenye Uwanja wa Emirates.
Kipigo
cha bao 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers maana yake timu hiyo haina nafasi ya
kubeba kwa miaka nane mfululizo sasa. Inaonyesha wana Arsenal kweli wamechoka.
Mwaka 2009,
Emmanuel Adebayor alijiunga Man City ada ya pauni milioni 25, nafasi yake
ikazibwa na Marouane Chamakh miezi 10 baadaye, kwa uhamisho usiokuwa na malipo
kutoka Bordeaux ya Ufaransa.
William
Gallas akatua Tottenham bila malipo, siku nne baadaye Sebastien Squillaci kutoka
Sevilla akatua Arsenal.
Mwisho wa
msimu wa 2010, Cesc Fabregas, Samir Nasri na Gael Clichy wakauzwa na nafasi zao
zikazibwa na Mikel Arteta, Gervinho na Andre Santos.
Msimu huu,
Robin van Persie kauzwa Man United kwa pauni 22m, halafu Wenger akamnunia Olivier
Giroud kutoka Montpellier ya Ufaransa kwa pauni 3m.
Kwa wote
wapya, angalau kidogo Arteta ameonyesha mafanikio, tena si kwa kiwango cha juu
sana.
Lakini Giroud
pia kajitahidi, wengine wote bado ni angalau tu, mfano; Santi Cazorla, Lukas
Podolski, Thomas Vermaelen, Alex Oxlade-Chamberlain na Per Mertesacker ni
wazuri lakini bado hawajaonyesha Arsenal imeweza kutibu ugonjwa wake.
Kinachoonekana
hapa Wenger anapoteza wachezaji wa kiwango cha juu zaidi halafu anachukua wale
wa bei nafuu na kuwatengeneza.
Uongozi
hauna tatizo naye, hakuna makombe lakini faida inaingia kubwa. Mashabiki hawataki
kuelewa hadithi za faida bila ya makombe.
Ndiyo maana wengi wanaingia katika
mjadala, inaonekana Wenger ndiye adui wa watu wote hasa mashabiki wa Arsenal.Ila kichekesho, wakati mashabiki wanataka aondoke, uongozi unaonyesha tayari kumuongezea mkataba wa miaka miwili. KAZI IPO.
0 COMMENTS:
Post a Comment