December 28, 2014


MPIRA UMEKWISHA
Dk 90+1 Javu anawatoka mabeki wa Azam FC, lakini anashindwa kuingiza ndani
Dk 89, Azam wanamuingiza David Mwantika
Dk 88 mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja kila upande ukionekana kuwa makini sana

Dk 83, Oscar analambwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Himid Mao

Dk 82, Yanga wanamtoa Tambwe anaingia Mrisho Ngassa
Dk 73 Yanga inamtoa Mrwanda, anaingia Hussein Javu

Dk 72, Juma Abdul anapiga shuti kalilaini MWadini anaokoaDk 70, Mwadini anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Msuva
GOOOOOOO DK 65 mpira wa kwanza Bocco anafunga bao kwa kichwa kwa krosi safi ya Himid Mao

Dk 64 Azam FC inamtoa Salum Abubakari na kumuingiza John Bocco 'Adebayor
Dk 57 Nyoni anapewa kadi ya njano kwa kumkata ngwara Niyonzima



Dk 53 Azam FC wanamtoa Kipre na nafasi yake inachukuliwa na Amri Kiemba



GOOOOOOOOO Dk 52 Msuva anafunga kwa kichwa kwa pasi ndefu ya Niyonzima

Dk 48 mwamuzi anampa Tambwe kadi ya njano kwa kumchezea faulo Wawa

Dk 46, Yanga inamtoa Edward Charles na nafasi yake inachukuliwa na Oscar Joshua
MAPUMZIKO
Dk 43 anageuka na kupiga shuti kali lakini kipa Mwadini anaokoa na kuwa kona

Dk 42 Yondani anapewa kadi ya njano kwa kumkata mtama Kavumbagu
Dk 39 Msuva anamzidi ujanja Kapombe na kupiga shuti kali lakini linadakwa na Mwadini.

Dk 35 Msuva anaifungia Yanga lakini mwamuzi anasema kipa amefanyiwa faulo.
Dk 33, Sherman anawapita mabeki wa mabeki watatu wa Azam lakini anapiga shuti mtoto

DK 28, Mwanaijege anapiga kona lakini kichwa alichopiga Kavumbagu kinatoka nje kidogo.
Dk 22, Tchetche anapiga shuti vizuri linatoka nje kidogo

Dk 21, Sherman anapata nafasi lakini anashindwa kuutumia vizuri
Dk 20, Wawa anaunganisha vizuri mpira wa kichwa lakini unatoka nje kidogo tu


Dk 19, Tchetche anapiga shuti kali lakini Dida anaokoa na kuwa kona.
Dk 8, Yanga wanachanganyana tena lakini shuti la Kavumbagu linagonga mwamba.

GOOOOOOO Dk 7, Tambwe anasawazisha kwa kichwa baada ya kuiwahi krosi ya Salum Telela

GOOOOOOO Dk 5 Kavumbagu anafunga baada ya mabeki wa Yanga kuchanganyana na kipa Dida
Dk ya 4 sasa, hakuna timu iliyofanya shambulizi kali na inaonekana timu zinacheza katikati uwanja zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic