Pamoja na kuwa na Simon Msuva na Mrisho
Ngassa, Kocha Hans van der Pluijm ameutaka uongozi wa Yanga kuongeza kiungo wa
pembeni mwenye kasi.
Pluijm raia wa Uholanzi ameueleza uongozi wa
Yanga kuwa anataka kiungo mwenye kasi kwa ajili ya kuimarisha kikosi.
“Kocha ametaka kuongezewa kiungo mwingine
mwenye kasi. Suala hilo amelifikisha kwa uongozi naye ameambiwa apendekeze.
“Kati ya wachezaji aliowapendekeza ni kiungo
mmoja wa zamani wa Simba. Sasa suala linafanyiwa kazi.
“Pia tunaangalia sehemu mbalimbali, lengo ni
kuboresha zaidi kikosi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Kuhusiana na suala la usajili, Pluijm
amekuwa akisisitiza kwamba si wakati wa kuzungumzia kwa madai ni mapema mno.








0 COMMENTS:
Post a Comment