March 20, 2016


Azam FC imesonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga tena Bidvest ya Afrika Kusini, safari hii kwa mabao 4-3.

Katika mechi ya kwanza, Bidvest ilipoteza kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani Johannesburg. Safari hii imepata imepata mabao matatu lakini ikashindiliwa mengine manne. Maana yake Azam FC imevuka kwa jumla ya mabao 7-3.




Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche amefunga mabao matatu, hat trick na moja likapachiwa na nahodha wake, John Raphael Bocco.

Hata hivyo, Azam FC ilishindwa kuonyesha kiwango kizuri hasa katika ulinzi huku beki wake kisiki, Serge Wawa akionekana kupwaya.

Kwani pamoja na washambuliaji wake kufunga mabao manne, lakini safu ya ulinzi ya Azam FC ilionekana kutokuwa imara huku Bidvest wakifunga kwa ulaini kutokana na soka lao la kitabuni.

Bidvest waliotumia vijana zaidi, walicheza soka la kitabu au la kufundishwa zaidi na kufanya kila jambo lao kuonekana rahisi.


Azam FC nao walionyesha soka safi hasa kipindi cha kwanza, lakini mambo yalizidi kubadilika kila wanavyosonga mbele.

1 COMMENTS:

  1. Sasa hapo utaona jinsi wachezaji waliokomaa na vijana tofauti yao!
    Ukitaka ushindi muda huu tumia waliokomaa,ukitaka ushindi miaka kumi ijayo tumia waliokomaa kipindi hicho ambapo kwa sasa ni vijana.Bidvest wametumia vijana wakalimwa goli 7-3 ila kama wangetumia waliokomaa mambo yangekuwa tofauti.Nyie waandishi kama hujui hujui tuu hata ukitumia wazeee kama akina kazimoto!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic