March 18, 2016


Azam FC iko vizuri na maandalizi yanaendelea vizuri na wako tayari kwa ajili ya kuwavaa Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika mechi ya Kombe la Shirikisho, Jumapili.

Katika mechi ya kwanza jijini Johannesburg, Wits ililala kwa mabao 3-0. Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema kamwe hawatawadharau.

“Maandalizi yanaendelea vizuri sana na hatuwezi kuwadharau kwa kuwa mpira hakuna kinachoaminika. Kikosi kitakuwa makini na tutapambana hadi mwisho. Tunaamini tutakuwa tumepita baada ya dakika 90 za mechi ya Jumapili,” alisema.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV