March 14, 2016


Baada Azam FC kuitumbua jipu Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika mechi ya Kombe la Shirikisho, Kocha Mkuu wake mkuu Stewart Hall, amesema ndoto yake ni kuhakikisha anaifikisha timu hiyo hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Azam imejiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mashindano hayo, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wasauz hao katika mchezo wa ugenini uliopigwa juzi Jumamosi nchini Afrika Kusini.


 “Hapa ni mwanzo tu lakini malengo yetu makubwa ni kuona kuwa tunatinga hatua ya makundi ikiwa ndiyo hatua ya kwanza ambayo tunataka kufika na tuna imani jambo hilo litafanikiwa maana tuna kikosi kizuri ambacho kinaweza kuleta upinzani kwa timu mbalimbali.


“Lakini ushindi huu umetupa nguvu ya kuona kuwa tunaweza kufika katika hatua hiyo na kuweka rekodi kwa msimu huu kwani mara nyingi tunaposhiriki mashindano haya ya Afrika, tumekuwa tukijikuta tukitoka kwenye hatua za mwanzoni kabisa,” alisema Stewart.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV