March 14, 2016Maisha yanaweza kubadilika mara moja tu bila ya wewe kutarajia, ndivyo ilivyo mtokea binti aitwaye Rmarni Ellis, mwenye umri wa miaka 19 tu.

Yeye alikuwa mfanyakazi wa duka moja jijini London, bahati yake ikaanzia pale bondia maarufu na mwanamichezo tajiri kuliko wote duniani, Floyd Mayweather alipoingia pale.

Wakati akipata huduma, Mayweather akaonekana kuvutiwa na binti huyo. Mwisho “akachombeza” na sasa Rmarni yuko jijini Miami, Marekani.


Huko amekuwa akionekana akila raha pamoja na Mayweather na hakuna ubishi tena kwamba sasa ni wapenzi.

Wawili hao wamekuwa wakionekana wakila bata kupitia mtandao wa Instagram wa binti huyo.


Mkali huyo wa masumbwi anaonekana amefika kabisa kwani yuko huru kuonekana akijiachia na binti huyo.

PICHA KWA HISANI YA INSTAGRAM YA RMARNI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV