March 15, 2016


MANARA

Mkuu wa kitengo cha Habari cha Simba na Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara amekanusha taarifa kwamba alitoa taarifa kuwa mechi ya Coastal Union dhidi ya Simba wikiendi hii imeahirishwa.

Manara amesema ni uzushi ambao unasambazwa na watu wasiojulikana wenye nia ya kutaka kuwachanganya Wanasimba.

"Si kweli, mtu kaweka tu kwa makusudi sijui nia yake ni nini. Anataka kuwachanganya Wanasimba na huenda wanachanganywa na ushindi mfululizo wa Simba jambo ambalo hawalifurahii," alisema Manara alipozungumza na SALEHJEMBE.

"Ukweli mechi ipo na kikosi kinaendelea na maandalizi kama kawaida," alisisitiza.


TAARIFA ALIYOTOA MANARA KUKANUSHA:
Napenda kukanusha hyo taarifa inayotembea mitandaoni ikihusisha jina langu.eti mechi yetu imehairishwa.
Ni uongo unaozushwa na wapinzani wetu wanaotapapa na matokeo yetu kwa sasa.
Puuzen taarifa hyo.ni ujinga na ulofa uliochupia mpaka.

Haji manara
Simba nguvu moja


TAARIFA INAYOELEZWA KUWA NI YA UZUSHI:
Habari wanachama na mashabiki wa SIMBA, kwa sasa timu yetu iko vizuri na mungu akipenda huu ndio mwaka Wa mwisho wa sisi kuitwa wa mchangani, hivyo nawaomba muisapoti timu yetu popote iendapo,

Napenda kuwapa official taarifa kuwa mechi iliotakiwa ichezwe tarehe 19 march 2016, Dhidi ya COSTAL UNION, HAITAKUWEPO, mechi hii imekuwa postponed mpaka TFF watakapo tangaza itachezwa lini, hivyo wanachama wenzangu msije kupoteza nauli zenu bure kwenda TANGA, NARUDIA TENA MECHI HAITAKUWEPO, sambaza ujumbe huu kwa GROUP zote ulipo, 
SIMBA NGUVU MOJA
Imetolewa na Mimi Afisa habari wanu

Hajji S. Manara

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV