March 20, 2016


Kocha Steward Hall wa Azam FC, amesema anajua haitakuwa kazi rahisi dhidi ya Bidvest ya Afrika Kusini.

Timu hizo zinarudiana leo katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam FC ilishinda kwa mabao 3-0 ikiwa ugenini Johannesburg na inaelezwa Bidvest ilipumzisha baadhi ya wachezaji nyota kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Afrika Kusini dhidi ya Orlando Pirates.

Sasa imeshuka na kikosi kizima kuivaa Azam FC, na Hall anasema: “Kweli haiwezi kuwa mechi rahisi. Ushindi utakuwa una uhakika baada ya dakika 90 za Chamazi.

“Lakini hatuwezi kuwa na hofu na kikosi, hata tulipokwenda kucheza nao, tuliwaangalia kwa uzito huo huo na inawezekana safari hii tutawaangalia kwa uzito wa juu zaidi.”


Mechi hiyo itarushwa moja kwa moja na runinga ya Azam TV ili kuwafaidisha ambao hawatapata nafasi ya kwenda uwanjani, leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV