March 15, 2016


Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba wameendelea na mazoezi kujiweka vizuri zaidi kabla ya mechi yao dhidi ya Coastal Union.

Simba itaivaa Coastal ambayo ni timu iliyozifunga timu mbili vigogo Ligi Kuu Bara, yaani Azam FC na Yanga na zote kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambako itacheza na Simba.


Chini ya Kocha wake, Jackson Mayanja, Simba iliendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV