March 19, 2016


Shomari Kapombe ndiye beki anayeongoza katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane hadi sasa, lakini siri ya mabao yake ni mfumo wa 3-5-2 unaotumiwa na timu yake, Azam FC.

Kapombe ameliambia Championi Jumamosi kuwa, chini ya mfumo huo, imekuwa rahisi kwake kufunga na kama wakiendelea kuutumia anaweza kufunga mabao mengi zaidi.

“Siri ya mabao yangu ni mfumo wa kocha wetu Stewart Hall ambao ni 3-5-2, chini ya mfumo huu, natumika zaidi katika kushambulia tofauti na kukaba, ndiyo maana nafunga sana,” alisema Kapombe.

Chini ya mfumo huo, Kapombe pia amefunga bao moja katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini ambayo ilifungwa mabao 3-0 na Azam wikiendi iliyopita. 

Mabeki wa kati watatu ndiyo wanaotumika katika mfumo huo kwenye majukumu ya kuzuia na kuwaacha mabeki wa pembeni wakicheza kwa kushambulia muda mrefu.


 “Nitaendelea kufunga zaidi kwa kutumia mfumo huu ambao unanibeba kwani nacheza kama mshambuliaji na wala sikabi sana kwa kuwa kazi yangu inafanywa na wenzangu watatu ambao wanacheza nyuma muda wote,” alisema Kapombe aliyewahi kucheza Simba.

SOURCE: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic