March 20, 2016


Mshambuliaji nyota wa zamani wa Ajax na Barcelona, Patrick Kluivert amesema kocha Louis van Gaal anastahili heshima ya juu zaidi kuliko hats Jose Mourinho au Pep Guardiola.

Kluivert ambaye aliwahi kufundishwa na van Gaal akiwa Ajax na baadaye Barcelona, amesema pamoja na kwamba kocha huyo ana wakati mgumu lakini anastahili heshima hasa kutoka wachezaji vijana.


Mshambuliaji huyo ambaye pia aliichezea AC Milan kwa mafanikio alistaafu akiwa na miaka 32, pia ni kati ya waliowahi kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa.


Kluivert bado anaamini mawazo ya van Gaal yatafanya kazi Man United huku akimsifia kuwapandisha vijana 14 katika timu ya wakubwa akiwemo Marcus Rashford ambaye amekuwa akifananishwa sana na Kluivert.

DAIL MAIL.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV