March 19, 2016

APR WAKIJIFUA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR, JANA.


Kocha Mkuu wa APR, Nizar Khanfir amesema Yanga wasitarajie mteremko hata kidogo ingawa anajua pia itakuwa kazi ngumu kwao.

APR itakuwa mgeni wa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

KANFIR
Kanfir raia wa Tunisia amesema kilichowaleta Dar es Salaam ni kubadili yale matokeo ya kupoteza kwa mabao 2-1 wakiwa nyumbani Kigali.

“Tunataka kuonyesha katika soka lolote linawezekana. Tumejiandaa na tuko tayari kwa ajili ya mchezo,” alisema.

“Tuna uwezo wa kufanya vizuri, tunalijua hilo lakini tutapambana kwa kuwa haiwezi kuwa mechi rahisi. Hata Yanga wasifiri APR itaendelea kubaki vilevile kama Kigali,” alisema.


Wakati APR ilipoteza kwa mabao 2-1, huo ndiyo ulikuwa mchezo wa kwanza wa kocha huyo kuinoa APR.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV