March 20, 2016


Kocha wa APR, Nizar Kanfir amesema ni uzoefu tu uliizuia timu yake kutofuzu dhidi ya Yanga ambayo waliizidia kila kona.

Yanga na APR zilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, jana.

Kanfir raia wa Tunisia, amesema walikuwa wamewashika Yanga kila idara na wangeweza kuwafunga hata bao nne.

“Tulikuwa na nafasi ya kufuzu, tulikuwa na nafasi ya kufuta makosa ya mechi ya nyumbani ambayo tulipoteza. Lakini bado timu una vijana wengi na wanapaswa kujifunza,” alisema.


Katika mechi ya kwanza mjini Kigali, Yanga ilishinda kwa mabao 2-1, lakini jana APR ya Rwanda ndiyo ikakamata kila idara na kuipa Yanga wakati mgumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV