March 19, 2016
MPIRA UMEKWISHAAAA
-Yanga wanapoteza nafasi nyingine ya kufunga bao, Mwinyi akiwa katika nafasi nzuri lakini hakuangalia lango
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 90, APR wanaendelea kugongeana tena, Iranzi anapiga krosi nzuri lakini MWinyi anauwahi mpira na kumpa Mwinyi anayeokoa na kumpa MWashiuya lakini anafanya bla bla kwa kushindwa kumpa pasi nzuri Ngoma

Dk 88 Bayisenge anaingiza mpira mzuri ndani ya eneo la lango la Yanga, TWitte anaokoa. Sibomana anaurudisha tena lakini Mwinyi anapiga mbele kabisa

Dk 86, Ngoma anaingia akikabwa na mabeki wawili wa APR, lakini wanamwangusha na kuwa faulo
SUB Dk 82,anatoka Benedata Jamvier kwa upande wa APR na nafasi yake inachukuliwa na Betrand Iradukunda

 Mwashiuya anawahadaa mabeki wa APR na kupiga shuti kali kabisa. Lakini alishindwa kulenga lango
Dk 77, Mwashiuya anaonekana kuwa msumbufu kwenye ngome ya APR, lakini mabeki wake hasa Rwatubyaye anaonekana kuwa makini zaidi

Dk 70 hadi 74, APR wanaonekana kucheza vizuri zaidi wakimiliki mpira zaidi ya Yanga. Lakini hawako makini katika suala la umaliziaji
SUB Dk 69 Kaseke aliyeumia, anatolewa akiwa amebebwa kwenye machela na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
Dk 63 hadi 66, mpira unaendelea kuchezwa katikati ya uwanja. Yanga wanaonekana kama wameridhika pia na sare hiyo
Dk 62, krosi nzuri kabisa ya Jihadi lakini anawawahi washambuliaji wa APR na kuudaka mpira vizuri kabisa
Dk 60, MSuva anaingia moja kwa moja na kuchonga kona lakini APR wanaouondoa

SUB DK 60 Anaingia Msuva kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima aliyekuwa nahodha wa leo. Anampa Bossou kitambaa cha unahodha
Dk 58, Tambwe anajaribu kuingia kwenye lango la APR kwa kasi lakini Rutanga Eric anaokoa na kuwa kona.

Dk 54, Yanga wanagongeana vizuri. Hata hivyo bado ile hali ya timu kutaka bao si kubwa sana na zaidi ni ule mpira wa kugongeana
KADI Dk 52 Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kumzuia kipa wa APR kupiga mpira
Dk 49, Iranzi anaingia vizuri na kupiga shuti kali safi lakini Barthez yuko makini, anadaka

DK 48, Haji Mwinyi anapiga krosi nzuri kabisa lakini inakosa mmaliziaji, inabidi APR wawe makini
SUB Dk 46, APR wanamtoa mfungaji Fiston Nkinzingabo anaingia Jihadi Bizmana
Dk 46, mpira kipindi cha pili umeanza na kama kawaida, unaanza kwa kasi ya taratibu kabisa

MPIRA NI MAPUMZIKO
Dk 45, Kakusoko anachonga mpira wa faulo, hatariiiiii, mpira unapita juu kidogo ya lango la APR
Dk 44 hadi 45, APR wengi wanaonekana kurudi nyuma na zaidi wanajilinda kama vile sare kwao inawafaa zaidi
Dk 43, Kipa Ndoli anafanya kazi nzuri ya kuuwahi mpira miguuni mwa Tambwe. Kama angechelewa kutoka mapema ingekuwa habari nyingine kabisa

Dk 35, APR wanagongeana vizuri lakini Bossou anatibua hesabu zao na kuutoa mpira. Unakua wa kurushwa, unamkuta Iranzi, anapiga shuti kali kabisa lakini hakulenga lango
Dk 33, Bigirimana anajaribu shuti lakini bado anashindwa kulenga
Dk 31 hadi 36, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja huku APR wengi zaidi wakiwa nyuma kuhakikisha hawafanyi makosa tena

Dk 30, beki Lutanga wa APR analazimika kumwagusha Ngoma aliyekuwa amemtoka. Faulo ni nje kidogo ya 18
GOOOOOOOO Dk 28 Ngoma anampiga chenga 
Rutanga Eric na kupiga shuti kali la chinichini ambalo linamzidi Ndoli na kujaa chini
Dk 23 hadi 26, APR wanaonekana kutulia zaidi na kucheza vizuri wakiwapa Yanga wakati mgumu
Dk 22, Niyonzima anapiga krosi safi kabisa, Kamusoko anagonga kichwa, mpira unagonga mwamba na kurudi uwanjani, Ndoli anaudaka vizuri kabisa

Dk 20, mashabiki zaidi ya 25,000 waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa wanaonekana kuwa kimya kabisa kwa kuwa Yanga haijaonyesha soka zuri na APR ndiyo wanaonekana kushambulia zaidiDk 16, Bossou analazimika kutoa mpira na kuwa kona baada ya Benedata Jamvier kuingia vizuri. Iranzi anachonga kona lakini haina madhara kwenye lango la Yanga
 Dk 14, Yanga wanapata kona, inachongwa na Niyinzoma na Kaseke anauwahi mpira na kumkuta Mwinyi lakini anakuwa si makini katika umaliziaji

Dk 14, mpira safi wa adhabu unachongwa na Bayisenge lakini Barthez anadaka vizuri
Dk 11, Ndoli anaonyesha ujuzi kwa kudaka shuti la Tambwe aliyekuwa katika nafasi nzuri
Dk 9, Tambwe anapoteza nafasi ya kwanza ya Yanga, aliunganisha mpira kabisa wa Twite lakini akashindwa kulenga lango
Dk 8, hadi sasa Yanga hawajafanya la maana, wanaonekana kucheza kwa kubutua na hawajiamini au walioanza bila ya mipango na wanatakiwa kutulia

Dk 7, Sibomana nusura afunge tena baada ya mbeki wa Yanga kujichanganya na Bossou anaonekana kulalama 
KADI Dk 5, Niyomzima analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Rusheshangoga
GOOOOOOOOO Dk 3, Fiston Nkinzingabo anaunganisha krosi nzuri kabisa ya Rutanga Eric na mpira unajaa wavuni vizuri kabisa kwa ulainiii


Dk 2, Twite anakwenda kurusha mpira vizuri kabisa lakini Mukunzi anaugonga na kuwa kona inachongwa na Kaseke lakini Ndoli anadaka vizuri kabisa.

1. Ally Mustapha 
 2. Mbuyu Twit
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Pato Ngonyani
7. Haruna Niyonzima
8. Thabani Kamusoko
9. Donald Ngoma 
10. Amisi Tambwe
11. Deus Kaseke


&&&&&&&&&&&&&&


1. Jean Claude Ndoli
 2.Rusheshangoga Michael 
3.Rutanga Eric 
4.Rwatubyaye Abdul 
5.Bayisenge Emiry 
6.Yannick Mukunzi 
7.Fiston Nkinzingabo 
8.Benedata Jamvier 
9.Bigirimana Issa 
10.Iranzi Jean Claude 
                           11.Sibomana Patrick

SUB
Kwizera Olivier
Rwigema Yves
Usengimana Faustin
Nshutinamagara Ismael
Djihad Bizimana
Betrand Iradukunda
Ntamuhanga Tumaini

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV