March 18, 2016


Huu unawezekana ukawa mwaka wa neema kwa mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib ambaye licha ya kuonyesha uwezo mzuri lakini kuna taarifa kuwa yupo njiani kununuliwa kiatu kipya cha mpira chenye thamani ya dola 500 (zaidi ya Sh milioni 1) kutoka Uingereza.

Kiatu hicho kitanunuliwa na mdau ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba licha ya kuwa yeye ni mhusika mkubwa katika mchezo wa ndondi.

Mdau  ambaye jina lake linahifadhiwa, amekuwa akifurahishwa na uwezo wa Ajib na matokeo mazuri ya Simba, hivyo kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda Uingereza alimfuata Ajib na kumuuliza namba ya kiatu anachovaa na kumwambia atamletea.

“Amesema atamnunulia kiatu cha dola 500 ambacho kitakuwa kina jina la Ajib, kwa sasa huyo jamaa yupo Uingereza,” kilisema chanzo cha habari.


Alipoulizwa Ajibu juu ya uwepo wa taarifa hizo, alisema: “Jamaa aliniuliza ninavaa kiatu namba ngapi, nikamwambia, akasema ataniletea kiatu tu, lakini mambo mengine hayo unayoniambia mimi hakuniambia, tusubiri tuone.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV