March 16, 2016

MWAMBUSI
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amelazimika kuondoka kikosini na kurejea kwao Mbeya baada ya kupata msiba.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza Mwambusi atarejea Dar Jumamosi, siku ambayo Yanga itakuwa kazini kuivaa APR ya Rwanda katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa ikiwa ni baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Kigali, Jumamosi iliyopita.

Mwambusi alilazimika kuondoka juzi Jumatatu kwenda Mbeya kwa ajili ya kwenda kumalizia msiba wa binamu yake ambaye alifariki wakati kikosi hicho kikiwa nchini Rwanda wakati wakicheza na APR katika mchezo wa raundi ya kwanza ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2-1.

Mwambusi amesema atalazimika kuwa nje ya kikosi hicho kwa siku kadhaa kutokana na kusafiri kwenda Mbeya alikopatwa na msiba wa binamu yake.

“Kwa sasa mimi nipo nje ya timu kwa siku kadhaa ambapo nimesafiri tangu Jumatatu (juzi) nipo Mbeya huku nimekuja baada ya kupatwa na msiba wa binamu yangu, nimekuja kumaliza msiba tu.


“Kila kitu tayari kimeshafanywa maana alifariki wakati mimi nikiwa Rwanda kwenye mchezo wetu dhidi ya APR ya nchini humo, nitakaa huku kwa siku chache baada ya kupewa ruksa na viongozi wangu,”alisema Mwambusi.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV