March 18, 2016Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima, ni maarufu sana nchini Rwanda unapozungumzia mchezo wa soka.

Alijiunga na Yanga akitokea APR, lakini anasema katika mechi ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu hizo, anachotaka ni kuona timu yake inashinda.

"Yanga tumejiandaa kushinda, ikitokea kama nimefunga bao, kweli nitashangilia sana.

"Kweli japokuwa najua APR kuna marafiki zangu na jamaa zangu wengi lakini nitafutahi tukisonga mbele,” alisema.

Katika siku za hivi karibuni, Niyonzima anaonekana kurejea katika kiwango kizuri.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV