March 13, 2016


Kikosi cha KRC Genk kinaongoza kwa mabao 2-0 katika mechi yake dhidi ya Oostende katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, sasa ni mapumziko.

Mtanzania Mbwana Samatta amefunga bao la kwanza katika dakika ya 24 na Leon Bailey amefunga la pili katika dakika ya 39.


Hiyo ni mechi ya kwanza ya Samatta kuanza katika kikosi cha kwanza, nyingine tatu aliingia katika kipindi cha pili na moja akafunga dhidi ya Club Brugge.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV