March 18, 2016


TAMBWE
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, amesema APR wana kikosi bora lakini hawawezi kusalimika jijini Dar.

Hii ni michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Yanga ilianza mechi yake ya kwanza kwa kuifunga APR kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kikgali, Rwanda.

Mechi ya pili dhidi ya timu hizo zenye upinzani kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, inapigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Tambwe raia wa Burundi amesema si kazi rahisi kuwamaliza APR, lakini Yanga wamejipanga vilivyo.

“Safari hii tumejipanga, tunataka kufika mbali, tumejipanga kushinda mechi zote za nyumbani na hata zile za ugenini pia, ndiyo maana nina uhakika mechi na APR tutapata ushindi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV