March 20, 2016


Timu ya taifa ya soka ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mchezo uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Rufaro jijini Harare.

Twiga katika mchezo wa leo imecheza vizuri na kuweza kuwabana wenyeji katika uwanja wao wa nyumbani kwa kuwalazimisha sare, na weyeji kupata nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-2.

Kwa matokeo hayo Twiga Stars imetolewa kwenye michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

Kikosi cha Twiga Stars kinatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV