March 15, 2016


Uongozi wa Simba umesema utaendelea kutoa “full support” kwa Kocha Mkuu, Jackson Mayanga raia wa Uganda.

Uamuzi huo unatokana na namna kocha huyo alivyoonyesha juhudi kubwa katika kukibadilisha kikosi chake hata kuliko makocha waliopita, wakiwemo waliotokea barani Ulaya.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema uongozi utafanya hivyo ili kuhakikisha kikosi chao kinaendelea kupambana.

“Tunaona mchango wa wachezaji, tunaona mchango mkubwa wa kocha. Hakika lazima tuwaunge mkono kwa nguvu kabisa.

“Tuko pamoja na kocha kwa kuwa tunaona juhudi zake na uongozi umemuahidi kuendelea kumuunga mkono na itakuwa hivyo.

“Pia tuko pamoja na wachezaji na lengo letu ni kuona vijana wanapambana hadi mwisho. Hali ya timu inaimarika kila siku, jambo linalotupa moyo kuendeleza ushirikiano huo,” alisema Kaburu.

Mayanja aliingia Simba kama kocha msaidizi chini ya Dylan Kerr raia wa Uingereza ambaye alitimuliwa hata kabla ya Mayanga kuanza kazi.

Baada ya hapo, Simba ilisitisha kutafuta kocha mkuu baada ya kuona Mayanja alikuwa akifanya vziuri katika mechi zake zote za mwanzo, tena mfulilizo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV